Monday, May 6, 2013

MKUTANO WA PROF. MAGEMBE WAZIRI WA MAJI NUSURA ULETE BALAA KWA WANANCHI WA MJI WA MUGUMU –SERENGETI



MKUTANO WA PROF. MAGEMBE WAZIRI WA MAJI NUSURA ULETE BALAA KWA WANANCHI WA MJI WA MUGUMU –SERENGETI.
05/05/2013.
Waziri wa maji Mhe. Prof. Jumanne Magembe akiwa katika ziara ya Kiserikali ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo hasa katika sekta ya maji amefika leo katika wilaya ya Serengeti mkoani mara akiambatana na mbunge wa jimbo la Serengeti Mhe. Dr. Steven Kebwe pamoja viongozi wengine toka Sekretarienti ya maji toka wizarani. Pia Mhe. Magembe akiwa Serengeti ameambatana na timu ya watalaam toka sekretarieti ya maji ya mkoa wa Mwanza na viongozi toka Mamlaka ya maji safi na taka ya mkoa wa Mara ambao ndio wangalizi wa mradi wa Bwawa la Manchira la wilaya Serengeti.

Baada ya waziri kutembelea Bwawa la wa Manchira kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa juu wa serikali kila wafikapo Serengeti huenda kutembelea Bwawa hilo, majira ya saa 11 jioni aliwasili katika Mji wa Mugumu kwa ajili ya kuongea na wananchi waliokuwa wakisubiria kusikia kauli yake katika eneo la uwanja wa Mbuzi.

Kama ilivyo kawaida na desturi yetu watanzania, kabla ya kiongozi husika kusimama na kuongea na wananchi basi kunakuwepo na salamu na maneno ya hapa na pale toka kwa viongozi wenyeji na pengine wale walioambatana na kiongozi mkubwa, hii yote ikiwa ni kutaka kuweka vizuri hali ya hewa kwa maana ya kuandaa wananchi kumsikiliza kiongozi mkubwa pindi uadiapo mda wake wa kuongea.

Leo katika eneo la uwanja wa mbuzi ilikuwa hivi;
Kwanza kabisa alianza katibu Tarafa ndg. Shanyangi kuwasalimia wananchi kwa kusema Serengeti hoeeee! Wananchi hawkujibu chochote, tena akarudia salamu kama mara mbili mara tatu hivi Serengeti hoeeeeeeee, Magembe Safiiiiiiiiii, wananchi kimya na badala yake zilisikika sauti chache toka meza kuu sehemu walipoketi viongozi wa chama na serekali pamoja na waziri mwenyewe zikisema safiiii. Na mwisho katibu huyo alihoji mbona wananchi mnanyaza, kuna tatizo gani? Wananchi wakasema unalijua.

Baada ya hapo ndg. Shanyangi alimwita Mbunge Viti maalum na katibu wa UWT –Taifa aliekuwa ameambatana na waziri Magembe kuja kusalimia wananchi na kusema machache……pia hali haikuwa nzuri kwa mama huyo kwani alijikuta akiongea huku wananchi wakiwa na minongono ya hapa na pale, alijaribu kuwasihi hata kwa kutumia baadhi ya maneno ya kilugha kwa kutoa salamu pia haikuweza kuzaa matunda vizuri, ambapo mbunge huyu alijikita katika kuwambia wananchi kuwa kama wanangalia TV yeye ni mchangiaji mzuri bungeni na katika Bunge hili linaloendelea yeye amechangia mara 4 katika mambo mbalimbali ikiwemo kuwatetea wafanyakazi.

Baada ya katibu huyo alifatia kaimu Mkuu wa wilaya ya Serengeti ndg. Joshua Mirumbe ambae pia kama kawaida aliaza kwa kuwasalimu wananchi wa wilaya yake ne akambulia patupu lakini hakuishia hapo aliendelea kusema machache ya moyoni mwake kwa wananchi wake na kuwaomba wamsikilize waziri Magembe kwani amekuja na majibu ya matatizo yao hasa kero ya maji katika mji wa Mugumu na vijiji jirani, na baada ya hotuba yake fupi alisema sasa naenda kumwita Mbunge wa jimbo letu mhe. Kebwe hapo ndipo wananchi walianza kwa kuzomea na kupiga kelele za hapa na pale kwa kukataa kutomsikiliza mbunge wao………kwa kusema wooooooooh, hatutaki huyo hapanaaaaaaaa,

Baada ya kusikia maneno hayo Mkuu wa wilaya alipandisha jazba na kusema “hamtaki nini? Huu ni mkutano wa serikali mnaleta uhuni, hatutaki uhuni hapa, OCD nakwamuru simama na hakikisha wanaoleta uhuni hapa wanathitiwa mara moja, Serekali inawatea majibu ya matatizo yao then wao waleta upuuzi, alisema DC Mirumbe”. Na kwa kauli hiyo ya DC MIrumbe OCD alitoa ishara kwa askari polisi waliokuepo eneo hilo na walianza kutanda kwa kuzingira wananchi na wananchi waliokuepo walilazimika kuwa kimya na ndipo Mbunge alipo simama na kuongea na kwa hali isiyo ya kawaida Mbunge alianza kuhutubia bila kusalimiana na wananchi wake.

Mpka mwanablog hii anaondoka eneo hilo la mkutano, waziri Magembe katika hotuba yeke kwa wanamugumu alisema serekali kupitia wizara yake ya maji imetenga kiasi cha shilingi milioni mia tano (500,000,000/=) katika bajeti ya serekali ya mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mradi wa usambazaji maji safi na salama toka bwawa la manchira Serengeti , ambapo pesa hizo zinatarajiwa kutumika katika uwekaji wa tank la kuchunja na kutibu maji toka Bwawani, huku watalaamu wakisema kuweka chujio linaghamu kiasi cha Bil. 7, swali linabaki kuwa je hizi mil.500 za Magembe zitawasaidia wanasengeti kuondokana na tatizo la kunywa maji yasio safi na salama?

Mwisho………..

Swali: kwa nini hawa wananchi wanakataa kumsikiliza mbunge wao waliomchagua wenyewe?
Mpaka washurutishwe na mkuu wa wilaya?