Friday, October 4, 2013

MAUAJI YA KINYAMA - SERENGETI



Jana tarehe 03/10/2013 kulitokea mauaji ambayo yalimsibu mwendesha pikipiki maarufu kama Boda Boda ambae alichomwa na kisu eneo lambavuni na kumsababishia umauti. Dereva Boda boda huyu anafahamika kwa jina la Gwitembe Yagera anekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 -60, mwenyeji wa kijiji cha Kisangura kata ya Kisangura –Serengeti, alichomwa kisu na mtu anaesadikiwa alikuwa mteja wake ambae alimkodi katika hali ya kawaida kutoka Mugumu mjini ili ampeleke kijiji cha Masangola.

Wakiwa njiani kuelekea huko Masangola,walifika katika sehemu ambayo nikama kamsitu Fulani na sehemu ambayo siyo nzuri kupita kwa mwendo kasi wa pikipiki hapo ndipo abiria huyo alipomchoma na Kisu ambacho kinaonekana kwenye picha hapo chini na kumsababishia umauti marehemu mzee Gwitembe. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 marehemu alikuwa mgombea wa Udiwani katika kata ya Kisangura kwa tiketi ya CCM ambapo hata hivyo alishindwa kura na mgombea kwa tiketi ya Chadema.

Akiongea na mwana Blog hii mmoja wa waendesha pikipiki hao ambae pia ni katibu wa umoja wao ndg. Chacha Antony alisema wamesikitishwa sana na kitendo hicho na kusema anaviomba vyombo vya Dola likiwemo jeshi la polisi kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina na waharaka ili kumtia mbaroni mtu huyo aliehisika na kitendo hicho ili sheria iweze kuchukua mkondo wake. Kazi hii tunayofanya ni ngumu sana kiukweli ni Mungu tu anatulinda kwa sababu wewe unakuta huwelewi uliembeba analengo gani na wewe hata kama unamfahamu, kwa hivo tunafanya kazi kwa hofu sana "alisema mmoja wa madereva hao"

msafara wa pikipiki ukingia Mugumu mjini kutokea mosongo kuchukua mwili wa marehemu

Hospitalini Nyerere DDH, mwili wa marehemu ukingizwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti, mwili umo ndani ya gari la Polisi linaloonekana kwenye picha.

Kisu kilichotumika kuondoa uhai wa Marehemu Gwitembe, kisu hiki kilikutwa kimezamishwa ndani ya mwili wa marehemu

Mwili wa marehemu Mzee Gwitembe Yagera.


Pikipiki za wenzake zikiwa zimeegeshwa katika viwanja vya DDH