Tuesday, March 26, 2013

MAFUNZO MAALUMU YA UONGOZI NA USIMAMIZI BORA WA VYUO

Picha ya pamoja Wakuu wa Vyuo toka kanda mbalimbali za Tanzania walioshiriki mafunzo ya Uongozi, pamoja na wakufunzi toka chuo cha Walimu VETA Morogoro

Nikipokea Cheti cha kuhitimu mafunzo toka kwa Mkuu wa Chuo cha walimu VETA -Morogoro

Wakuu wa Vyuo toka kanda mbalimbali za tanzania

Eneo la chuo cha walimu wa VETA -Morogoro

Katikati ni Mkuu wa chuo cha walimu MVTTC, Ndg. ..........)kushoto kwake ni mkuu wa Taaluma na mafunzo wa MVTTC Ndg. Maro na kulia ni Mama Mweta ambae ni M/kiti wa wanasemina


Tuesday, March 5, 2013

HALIMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YADIMISHA SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA



SIKU YA MAZINGIRA AFRICA.
Kutokana na kuongezeka kwa Idadi ya watu katika nchi mbalimbali Duniani shughuli za kiuchumi nazo zinakuwa na kuongezeka kulingana na hali halisi ya watu (population), wakati Idadi ya watu ikiongezeka na shughuli za kiuchumi kwa kila nchi huongezeka na hali ya mazingira inazidi kuwa tete kwa kuchafuliwa kutoka na shughuli za uzalishaji za kila siku zinazofanywa eitha na mtu mmoja mmoja au Viwanda.

Kutokana na hali hiyo, Nchi wanachama wa Africa (AU) ziliona ni muhimu kuwa na utaratibu na mpango wa kuokoa mazingira katika nchi mwanachama wa AU. Nchi hizi kwa pamoja ziliridhia uanzishwaji wa wiki ya mazingira Barani Africa ambayo kilele chake huadimishwa kila tarehe 03 machi kila mwaka ambapo siku hii watu wote hutakiwa kushiriki katika shughuli za kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya makazi, maeneo ya Biashara kama masoko, Viwanda n,k hii ni kwa ajili ya kuyaweka mazingira safi kwa ajili ya ustawi wa Binadamu ambao afya zao zaweza kuwa hatarini kama matekeo ya mazingira kuwa machafu.

Siku hii ya mazingira barani afrika huadhimishwa na kila nchi mwanachama wa AU kupitia serikali zake, kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali, Asasi/Mashirika ya kiraia pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira ambapo hii inaweza kufanywa kwa staili tofautofauti kulinga na utashi wa Serikali na wadau wengine kwa kila nchi bila ya kubadili maana halisi ya siku hii ya machi,03.

HALIMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YADIMISHA SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA
Halimashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara kupitia Idara yake ya Mazingira imeadimisha siku ya usafi wa mazingira barani Afrika kwa watumishi wa halimashauri hii kutoka ofisini na kuungana na wananchi wengine kufanya usafi katika maeneo ya mji wa Mugumu ambao ni makao makuu ya halimashauri hiyo ya Serengeti.

Katika kuhakiki kuwa jamii inawelewa nini maana ya siku hii ya machi 03 H/M ilichukua jukumu la kuweka matangazo ya wazi yaliotangazwa kwa njia ya Vipasa sauti kuzungu mji mzima wa Mugumu na Vitongoji vyake kwa lengo la kuhasisha wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wakianzia na maeneo yao ya makazi (Nyumbani mwao) na pia kushiriki katika zoezi la pamoja la kufanya usafi kuzunguka mji wa Mugumu, zoezi ambalo liliongozwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti na mkurugenzi wa Halimashauri ya wilaya.

Katika utekelezaji wa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira watumishi wa halimashauri wamejitokeza japo kwa uchache kuungana na wananchi wengine, WANAFUNZI WA CHUO CHA UTALII CHA SERENGETI (SETCO) pamoja na WATUMISHI wengine wa chuo hicho wamejitokeza na kuungana na wafanyakazi wa halimashauri ya wilaya na wale wa kutoka katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Mugumu, wananchi wa kawaida wamejitokeza kwa uchache sana ambao idadi yao haikuzidi watu 15 ukilinganisha idadi ya watu walio katika mji wa Mugumu ambao ni zaidi ya watu 5000. Maeneo yaliopata bahati ya kufanyiwa usafi ni pamoja na eneo la soko kuu ambalo limefanyiwa usafi na wanafunzi na watumishi toka chuo cha SETCO na eneo la Uwanja wa mbuzi ambalo limefanyiwa usafi na watu wote akiwepo mkandarasi wa usafi wa mji wa mugumu ambae hata hivyo jina lake halikufahamika kwa haraka.

Nyenzo zilizotumika katika zoezi hili muhimu la usafi zilikuwa ni pamoja na; Panga, Majembe, sepeto, Rekki, mafekeo, mifagio, mikokoteni na Gari kwa ajili ya kubebea uchafu kwenda jararani. Watu walifanya kazi ya kufyeka, kuokota na kupeleka uchafu jararani.

MKUU WA WILAYA AONGEA NA WANANCHI:
Mara baada ya zoezi la usafi kumalizika kwa mujibu wa ratiba iliokuwepo Kaimu Mkuu wa wilaya ambae pia ni Afisa tawala wa wilaya ya Serengeti alipata fursa ya kuongea na wanachi kama sehemu ya kutoa maagizo ya Serikali kuhusiana na siku hii ya mazingira Afrika. Akiongea na wananchi kaimu mkuu wa wilaya Bw. Zonzo alisema kila mwananchi kwa nafsi yake ana jukumu la kulinda na kuweka mazingira safi kwa ajili ya ustawi wa jamii, alisema kwa kuwa shughuli za kiuchumi zinaongezeka mazingira yanakuwa katika hatari ya kuharika kutokana na shughuli hizo hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuona umuhimu wa kulinda mazingira kwa kufanya usafi kama inavyotakiwa.

Bw. Zonzo hakuishia hapo ila alisema pia wadau wa mazingira wafanye jitihada za kuendeleza maeneo ya wazi katika mji wa Mugumu akitolea mfano eneo la uwanja wa Bunzi kuwa linafaa sana kuwekewa Bustani (Garden) ya kupumzikia watu huku wakipata kinyaji bila kutaja ni kinywaji cha aina gani. Mkuu wa wilaya pia amekerwa na tabia ya wananchi walio wengi kupuuzia swala hili la usafi wa mazingira ambapo watu hawakutokea na badala yake walibaki kuwashangaa wale waliokuwa wakifanya zoezi la usafi, Mkuu huo aliongeza kwa kibwagizo kidogo kuwa “nashangaa kuona watu wanambia kuhusu habari ya kufanya usafi hawajitokezi badala yeke wamebaki kuwashangaa nyie mliojitokeza lakini wangeambia mtu kashikwa ugoni hapa uwanja ungepungua “ alisema

Mwisho mkuu wa wilaya alimaliza kwa kutoa ushauri ambao kimsingi ulichukuliwa kama agiizo rasimi la serikali kuwa wilaya kupitia wataalamu wake wa mazingira wafanye utaratibu wa kufanya usafi wa mazingira kwa kila wiki, pia aliagiza watu ambao ni vinara wa kuchafua mazingira wakamatwe bila ya kuwaogopa na wafikishe mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake, “watuwezi kuvumilia watu wanachafua mazingira wazi wazi huku hawachukuliwi hatua zozote kwa sababu wao ni maarufu hapa mjini” alisema Bw. Zonzo

wanafunzi wa chuo cha SETCO wakiokota Uchafu eneo la soko kuu mjini mugumu

usafi eneo la uwanja wa mbuzi

Soko kuu wanafunzi wa STCO wakizoa uchafu

wa kwanza kushoto ni kaimu DC serengeti Mr. Zonzo, katikati baada ya mwanamke ni kaimu DED serengeti wa kwanza kulia ni Afisa Mazingira wilaya Victor Charles







Afisa wanyama pori W Mr. Cathbet Boma akifyeka eneo la uwanja wa mbuzi