Leo tarehe 13/10/2015 kumekua na mkutano wa kitaifa wa kampeni za chama cha mapinduzi ccm uliofanyikia katika viwanja vya mbuzi mjini mugumu wilayani serengeti. katika mkutano huo viongozi wa juu chama chama hicho wamehutubia mamia ya wakazi wa mji wa mugumu na viunga vyake, viongozi hao alikua ni Mwigulu L. Nchemba amabe ni Naibu katibu mkuu ccm Tz bara na naibu waziri wa faedha na mwingine alikua ni Dr. Anthony Dialo ambae ni M/kiti wa ccm mkoa wa mwanza.