KAMBI YA
KITALII YAUNGUA MOTO, ROBANDA –SERENGETI.
Na Samwel
M.P
Leo siku ya J`mosi tarehe 05/09/2015 majira ya saa 5 asubuhi
kuelekea saa 6 mchana, baadi ya majengo ya kambi ya kulala watalii ya Ikoma
Safari Camp maarufu kama kwa Pepe iliyopo katika kijiji cha Robanada wilaya ya
Serengeti yameteketea kwa moto. Mwandishi
wa Blog hii ameshuhudia kwa macho tukio hili ambapo alifika kambini hapo akiwa
katika ziara yake ya kutembelea wadau wa Utalii hasa kambi za kulala wageni na
kufanya mazungumuzo na uongozi na hata wafanyakazi wa kawaida wa kambi
zinazopatikana eneo la Robanda na Ikona WMA.
Alipofika alikuta moshi mkubwa wa moto umetanda uliokuwa
umesababishwa na kuungua kwa majengo hayo ya Kambi hiyo ya IKOMA Camp (kwa
PEPE). Akiongea na mwandishi wa blog
hii, Meneja wa Kambi hiyo Bi. Tonel Brite amesema kuwa hata yeye anashindwa
kubainisha kuwa ni nini chanzo cha moto huo kwa sasa mpaka pale uchunguzi
utakapofanywa na timu ya wataalam wa majanga ya moto itakayokuwa imetumwa na
kampuni inayomiliki Kambi japo tetesi za awali zinaonyesha kuwa ni hitilafu
katika vyombo vyao vya umeme. Brite kwa maelezo yake mengine ya awali alisema
kuwa yeye alikuwa ndani akiendelea na kazi ya kupitia vitabu vya mauzo na
mlinzi aliekuwa zamu alikuwa ameenda kuzima mashine inayosukuma maji toka
kisimani kuja kwenye kambi, ambapo mlinzi huyo wakati anaudi ndipo aliona moshi
ulioashiria moto na alipoenda kuona alikuta tayari moto umeishaanza kuteketeza jengo
na umeshika katika nyasi zilizotumika kuezekea majengo.
Mlinzi huyo ambae jina lake halikuweza kufahamika alimtaarifu
meneja kuwa kuna moto na meneja pamoja na wafanyakazi wengine wa kambi hiyo
walipiga (mwenu) yoe au kelele kwa kuwaita watu ambao wako maeneo jirani na
kambi hiyo kwa ajili ya kuomba msaada wa kudhibiti moto; majirani wa kambi
walijitokeza na kusaidia baadhi ya vitu vichache toka kwenye majengo yaliokuwa
yameshika moto. Kwa mujibu Bi, Brite ambae ni meneja wa kambi, amesema kuwa
vifaa vingi vimeteketea kwa moto, na kusema jingo lililoteketea ni ambalo
linatumika kama Baa, Bwalo la chakula (Mesi) na Jiko. Haya ni maeneo ambayo
yanakuwa na vifaa vingi vya huduma, mapambo ya gharama, fenicha (Samani), n.k hivyo
ndiyo maana nasema vitu vingi vimeungua alisema Brite.
Hakuna mtu yeyote alieripotiwa kujeruhiwa au kupoteza maisha
kutokana na moto huo. Kuhusu hasara ambayo kambi hiyo imeipata kutokana na janga
hilo la moto Bi. Brite amesema haizi kulisemea hilo kwa sasa mpaka pale
tadhimini itakapofanywa badae na uongozi wa kampuni. Pia ikumbukwe kuwa miezi
kama 2 iliopita, aliekuwa meneja msimamizi na mwanzilishi wa kambi hiyo Bw.
PEPE alifariki dunia hivyo bado wafanyakazi wanamajonzo ya kuondokewa na
mwanzilishi wa kambi hiyo.
Kutokana na ziara ya mwandishi wa Blog hii ya kutembelea
kambi zinazopatikana Robanda, nyingi zimeonekana kuwa katika hatari kubwa ya
kunguua moto kutokana na uchomaji wa moto unaofanywa na watu wasiojulikana
kwenye maeneo yanayozunguka kambi hizo. Uongozi wa kambi hizo umedai mara
nyingine moto hutokea ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mwingine
kuchomwa na wanakijiji kwa lengo la kuchoma mkaa na kuweka mitego yao ya kunasa
wanayama aina ya Swala ambao huvutiwa na nyasi change zinazochipua baada ya
kuchoma moto. Tunakosa amani na tunakosa raha kwa hofu ya moto hasa nyakati za
kiangazi kikali, moto unaibuka gafla ni changamoto kubwa sana alisema Bw.
Timoth wa Mapito camp
 |
| Jengo la Restaurant ambalo lilikua na kigorofa likiwa limeteketea kwa moto |
 |
| Wanakiji wakiwa wanaendelea kuokoa vyombo mbalimbali toka ndani huku wengine wakianza kulewa kwa kunywa mivinyo ilikutwa Baa, wengine wakila matunda na kulamba sukari ili waongeze nguvu ya kuukabili moto |
 |
| Vyombo vinaendelea kutolewa nje, kama inavyoonekana. |
 |
| Sasa siyo gorofa tena ila ni majivu |
 |
| Kazi ni moja tu kuzima moto. |
 |
| Niwahishie maji, alisema huyo mzima moto. |
 |
| Charle nae alikuwepoo |
 |
| Moto lazima uzimike. |
.