Saturday, September 3, 2016

TATIZO LA MAJI MUGUMU/SERENGETI BADO NI KITENDAWILI.



TATIZO LA MAJI MUGUMU/SERENGETI BADO NI KITENDAWILI.

Na Samwel M.P

03/09/2016

Ndivyo tunavyoweza kusema kuwa tatizo hili la maji katika mji wa Mugumu na viunga vyake kuwa sasa ni kitendawili amabacho kinahitaji kuteguliwa na mamlaka zote husika kwa haraka  ili kuwanusuru wananchi na hatari ya milipuko ya magonjwa amabayo yanaweza kujitokeza kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani. Lakini pia inavyoelekea kitendawili hiki kinaweza kisiteguliwe kwa wakati kama hakutakuwepo na msukumo/shinikizo la kutoka kwa wananchi wenyewe ambao ndio wahanga wa tatitizo hili kwa kusaidiwa na mwakilishi wao bungeni ambae ni mbunge wa jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba, Serengeti ONLINE imebaini.

Kwa mujibu wa taarifa ya mhandisi wa maji wilaya, Eng. Marwa Mlaza, tatizo hili la kukosekana kwa huduma ya maji kwa wananchi wa Mugumu, lilianza tangu tarehe 09/05/2016 ambapo pump ya kusukuma maji toka bwawa la manchira iliungua. Mchakato wa kupata mkandarasi na kuwagiza pump mpya na motor chini ya mamlaka ya maji Musoma –MUWASA ulifanika na hadi sasa zoezi hilo halijakamilika kutokana na motor kungua mara mbili. Hivyo basi ifikapo tarehe 09/09/2016 itakuwa imekamilika miezi 4 mfululizo sawa na siku 120 bila maji kwa wananchi na wakazi wa mji wa Mugumu, jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na mazingira yake vilevile.

Leo sept. 03, mwandishi wa blog hii ametembelea Manchira ambako kulitarajiwa kuwa na zoezi la kufunga motor kwa ushirikiano wa watalaam toka wizara ya maji (Dsm), MUWASA (Musoma), Supplier wa Motor (Arusha) na mafundi wa MUGUWASA na H/Mashauri ya wilaya Serengeti; zoezi hili limeshindwa kufanyika na watu kutawanyika kutokana na sababu zifuatazo kama ilivyoelezwa:-

1)   Hapakuwepo na mwakilishi au mtalam toka upande wa supplier wa motor kutoka arusha, na alipotakiwa kutoa ithini ili mafundi wa wizara na MUWASA kuendelea na ufungaji wa motor alikubali kwa maneno kupitia simu, na badae wakamuomba akubali kwa  maandishi kupitia barua pepe (email) kama sehemu ya kuweka kumbukumbu, mkandarasi alikataa na kusema wamsubiri hadi siku ya jumatano  Sept. 07 ndiyo anaweza kutuma mafundi wake kuja Mugumu jambo ambalo pia linaweza kuwa sii la ukweli kama ilivyodaiwa kuwa amekuwa akiahidi uongo mara nyingi.

2)   Ilionekana kifaa cha mambo ya umeme (circuit breaker) chenye capacity ya 180 A brand ya ABB ambacho kinatakiwa kufungwa kwenye mfumo wa umeme wa motor hiyo pia hakipo, na kilitakiwa kuwagizwa aidha Musoma au kuingine; hii ni baada ya mkandarasi kuwambia kuwa amekituma kwa ndege toka arusha kuja seronera na baada ya kufika seronera kwa bahati mbaya tena ndege imerudi nacho arusha baada ya kukosewa jina la mpokeaji.
3)   Tatu, ilikuwa tu ni vifaa vingine vidogo vidogo vilivyoshauriwa na mtaalam toka wizani kuwa ni vyema vikafungwa hapo ili kukomesha tatizo hilo kujirudia hasa katika mfumo wa umeme, vitu ambavyo pia inaonekana vinahitaji fungu Fulani ili kuletwa.

Katika mahojiano ya hapa na pale, ilionekana kuwa Mkurugenzi wa MUWASA ndiye anapaswa kumbana mkandarasi kwani MUWASA ndiyo iliyosaini mkataba na mkandarasi. Akiongea kwa masikitiko mwakilishi wa wizara ya maji (jina halikupatikana) amesema, MUWASA ni mamlaka kamili, hivyo wao kama wizara wanakosa nguvu ya kuingilia jambo hilo na kumforce mkandarasi, ila watajaribu kumshauri MUWASA kuona namna ya kumbana supplier ili afike mapema badala ya hiyo anayosema jumatano; na timu yake ya wizara haitondoka mpaka tatizo limekuwa solved; huku akihofia kuwa endapo itafika sept. 06 kabla ya maji kutoka, kuna hatari ya waziri wa maji kupata wakati mgumu bungeni toka kwa Mbunge wa Serengeti.

Pamoja na mambo mengine, watalamu wa wizara na Muwasa pia kila mmoja wameonyesha kushangaa jinsi wanamugumu walivyo kimya  huku wakiwa na tatizo kubwa kama hili. Mmoja wao amesema yeye alikusudia angefika akakuta (Nyomi ya watu) yaani kundi kubwa la wananchi wakiwa bwawani kama sehemu ya kudai kupata huduma ya maji, kama alivyowahi kushuhudia katika miji mingine aliowahi kufika kwa kesi kama hii. “Miezi 4 bila maji sii jambo dogo”, alisema. Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, motor haikufungwa na kila mmoja alionekana kumtupia lawama supplier na mafundi wote wa muwasa na wizara wameondoka kuridi musoma hadi siku watakapofika mafundi wa supplier.

==Mwisho==
Kazi inaendelea.

Gari ya MUWASA iliokuja na mafundi wa MUWASA na wale wa kutoka wizara ya maji (dsm)

Baada ya zoezi kuahirishwa, kazi ikawa ni kurudisha motor stoo


Makatibu wote wawili wa Mbunge, wa kiwasaidia mafundi kurudisha motor stoo, inaonekana ndogo ila ina uzito karibu 300kg



Monday, February 15, 2016

SIRI YA UWANJA WA NDEGE WA SERENGETI YAFICHUKA.



Kwa zaidi ya kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita, wananchi wa wilaya ya Serengeti na mkoa wa Mara kwa ujumla wamekuwa wakiishi kwa matumaini ya kupata uwanja wa ndege wa kimataifa (International Airport) au wenye hadhi ya kati (Standard airport); ambao kwa mujibu wa kauli za wanasiasa na viongozi wa halmashauri ya (w) Serengeti,  ulikuwa ujengwe katika kijiji cha Burunga, kata ya uwanja wa ndege ambayo imo ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu kilometa chache toka hifadhi ya taifa ya Serengeti. Uwanja huu wa Serengeti ulikusudiwa kuwa moja ya vichocheo vya ukuaji wa maendeleo hasa katika sekta ya usafirishaji na Utalii ndani ya wilaya ya Serengeti, mkoa wa Mara na hata kanda ya ziwa kama mradi huu ungeweza kutekelezwa pamoja na barabara ya makutano- Natta –Mugumu –Klensi – Loliondo Arusha kama wananchi walivyokuwa wakiahidiwa katika majukwaa.

Kilichojiri leo (15/02/2016) katika kikao cha baraza la madiwani wa H/m ya (w) Serengeti ambacho kimeketi kwa ajili ya kupitia na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya H/M kwa mwaka wa fedha 2016/2017, jambo hili la uwanja wa ndege wa Serengeti limeibuka kwa sura ambayo haikutegemewa na kuleta hisia tofauti na maswali mengi kwa wananchi na hata madiwani wenyewe. Hii ni baada ya diwani wa kata ya uwanja wa ndege Mhe. Daniel Kegocha (CCM) maarufu kama (Maisa) kutaka kupata ufafanuzi wa kina toka kwa katibu tawala wa mkoa Mara ambae alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhusiana na kukwama kwa utekelezaji wa mradi kwa mda mrefu na kusadikiwa kuwa mradi huo unakwamishwa na uongozi wa mkoa hasa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara, pamoja na kwamba taratibu zote zilishakamilika.

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo, RAS – Mara amesema kuwa, jambo hilo la uwanja wa ndege halipo mkoani na wala ofisi ya RC haina nia yoyote mbaya ya kukwamisha mradi huo kama inavyodaiwa isipokuwa bado jambo hilo liko halimashauri ya Serengeti. RAS akasema mkoa unashughulika na uwanja wa Musoma ambao ni miongoni mwa viwanja 12 vya ndege vya Tanzania ambavyo vilingia katika mpango wa kujengwa kupitia mkopo wa World Bank ukiwemo uwanja wa ndege wa Bukoba ambao amesema umeishajengwa. Akaongeza kusema kuwa serekali kuu haiwezi kujiingiza katika swala ambalo bado halijatimiza vigezo kwa maana ya kufuata taratibu zote husika kama inavyotakiwa kisheria.

WITO wa RAS kwa halmashauri ya Serengeti: ameushauri uongozi wa H/M kupitia baraza hilo kuwa, kama h/m inapenda kufanikisha jambo hilo wawe na vitu vifuatavyo;

  1. Mkataba halali baina ya H/M na mwekezaji alieonyesha nia ya kusaidia ujenzi wa uwanja na uonyeshe wazi ushiriki (commitment) ya mwekezaji na uonyeshe wazi mwekezaji anagarimia asilimia ngapi za gharama za mradi 
  2. H/M ionyeshe chanzo kingine cha fedha za kugarimia mradi na nikiasi gani ambacho wanakusudia kukipata toka kwa chanzo hicho ambacho kinaweza kuwa ni pamoja na wadau wengine wa maendeleo toka ndani na nje ya wilaya. 
  3.   H/M ipeleke ombi hilo TAMISEMI, lipite tume ya Mipango, lipite kwa idara inayohusika na utekelezaji wa miradi ya ubia (PPP), mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) n.k

Ameongeza kwa kusema kuwa endapo hayo kifanyika basi itakuwa ni rahisi kwa jambo hilo kuweza kusonga mbele kwani litakuwa limeeleweka muundo wake na kupata Baraka zote. Nawashauri jambo hilo lifanyike by 2018/2019 kwa sababu kwa sasa 2016/17 mda umeisha. “amesema RAS”

Baada ya melezo hayo ya RAS, hakuna diwani aliyeweza kutoa mchango wowote kuhusiana na swala hilo pengine kwa jinsi anavyolifahamu kutokaa na ushahidi wa mambo mbalimbali yaliowezakuwa yakifanyika hapo awali kwa ajili ya swala la uwanja hasa madiwani waliokuwepo katika kipindi cha awamu iliopita na sasa wamefanikiwa kurudi kwenye baraza; wote walikua kimya. Lakini pia baada ya maelezo hayo ya RAS imeonekana dhahiri kuwa jambo hilo la uwanja wa ndege Serengeti bado ni wazo (Idea) ambalo lilikuwemo na limo ndani ya vichwa vya watu Fulani au viongozi wa juu wa h/m, lakini wao wakalileta kwa wananchi kwa sura kama ni kitu ambacho kikotayari na kinaenda kuwa implemented soon, kama kweli hakuna zengwe lolote nyuma ya pazia.

MASWALI YA WANANCHI:

  1.   Kama ndivyo ilivyo, je ni kwa nini viongozi walionekana kufanya ziara za kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji wa viwanja kana kwamba swala hilo liko tayari?
  2.    Je walikua wakitumia fedha za umma au zao binafsi katika kufanya ziara hizo?
  3.    Je uko wapi mkataba pamoja na file lote la mradi uliosemwa kuwa tayari h/m ina mkataba na mwekezaji katika kujenga uwanja wa Serengeti?
  4.    Je ni kwanini h/m iliamua kufidia wananchi wa Burunga kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege Serengeti? 
  5.    Kama hapo awali ilionekana kuwa taratibu zimekamilika kiasi cha kutangazia wananchi je, inakuaje leo inaonekana hakuna kilichofanyika?

Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la h/m hayo ndiyo maswali ambayo wananchi na madiwani wapya walikuwa wakijihoji na kutaka ipatikane namna ya kupata majibu ya maswali hayo toka kwa viongozi wanaofahamu swala hilo.