Thursday, July 18, 2013

MGAO WA MAJI WATIKISA MJI WA MUGUMU.



Katika kipindi cha takribani wiki mbili zilizopita hadi hivi sasa kumekuwa na tatizo la uhaba wa maji ya bomba katika mji wa mugumu wilayani Serengeti pamoja na kuwepo kwa Bwawa kubwa la Manchira jambo ambalo limeweza kusababisha usumbufu kwa wateje/wakazi wa mji wa Mugumu wanaotumia maji yanayotoka Bwawa la Manchira na kusambazwa na Mamlaka ya maji safi na taka ya Mugumu (MUGUWASA).

Tatizo hili limekuwa likitokea kwa staili tofauti tofauti ambapo mda mwingine maji yanatoka katika mabomba kwa mda wa saa1 hadi masaa 3 na badae kukatika gafla kwa masaa mengi wakati wa mchana mida ya usiku huduma hii ya maji huwa haipo kabisa. Swala hili limeonekana kuwakera wateja wengi na kulalamikia mamlaka ya MUGUWASA na kuiona kama imeshindwa kutekeleza wajibu wake kama inavyotakiwa.  Akiongea na mwana Blog hii mteja mmoja amesema yeye anashindwa kujua kinachondelea dhidi huduma ya maji Mugumu, na kama ni mgao basi MUGUWASA wanapaswa kutoa ratiba kamili ya mgao ili mteja aweze kujipanga namna ya kubana matumizi ya maji kuliko kuwa kimya.

Swala hili limemfanya mwanablog hii kutinga katika ofisi za Mamlaka ya maji safi na taka za MUGUWASA na kuonana na uongozi na kujua zadi kuhusu kulalamika kwa wateja wao.  Katika ofisi ya MUGUWASA ameongea na Meneja wa Mamlaka Bw. Munema B.M, ambapo meneja amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema sii tatizo la kiufundi au Bwawa kuishiwa maji bali ni mgao wa maji unaendelea ambao chanzo chake ni kuongezeka kwa wateja waliounganishiwa huduma ya maji.

Akizungumuzia hali hii ya mgao, Bw. Munema amesema kuwa hii inasababishwa pia na uwezo wa tanki la kuhifadhia maji kuwa mdogo ambapo tanki lina uwezo wa kuhifadhi lita za maji 675,000 ambazo ni sawa na mita za ujazo 675M3 na uhitaji wa wateja ni mita za ujazo 1500M3 kwa siku.  Hivyo basi katika kutatua tatizo hili ni mpaka kujengwa kwa tanki lenye uwezo mkubwa wa kubeba maji ambapo amesema tanki la ujazo wa 10,000M3 linaweza kusadia kupunguza au kuondoa tatizo hilo la mgao wa maji kwa mji wa Mugumu na vitongoji vyake. Pia aliongeza kuwa analazimika kutoa huduma hii kwa mgao ambao kimsingi haujatangazwa na kufamika kwa wateja kuwa ni kulinda mashine inayosukuma maji toka bwawa la manchira kwenda kwenye tanki kwamab analazimika kuzima mashine hiyo ili kupumzika  kutokana na kufanya kazi kwa mda mrafu.

Alipoulizwa kuhusu bajeti ya serekali kwa mwaka huu kupitia wizara ya maji kama itasaidia kuondoa tatizo hili,Bw. Munema alisema yeye anasikia waziri mwenye dhaman na wizara husika alitenga  shilingi 500 milioni ambazo yeye hajui kuwa zimelenga kufanya nini kwa sababu ni ndogo ukilinganisha na uhitaji uliopo, ambapo alibainisha kuwa mahitaji ni zaidi ya shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa tank na chujio la maji. Ifahamike kuwe maji yanayotoka bwawa la manchira bado yanatumika bila kuchujwa.

Kuhusu kukatiwa umeme na Tanesco kwenye mashine ya kusukuma maji kwenda kwenye tanki, meneja alisema kuwa Ankara ya umemeni kubwa ambapo kwa mwezi hutakiwa kulipia Ankara ya umeme shilingi 7milioni, na hali pale yeye makusanyo yake ya Ankara za maji toka kwa wateja ni kama shilingi 6milioni. Katika hizi 6 mil hupaswa kulipa vibarua wanaofanyakazi na MUGUWASA na matumizi mengine ambayo hakuyafafanua, hivyo basi hii inakuwa ni changamoto kwa mamlaka kushindwa kulipa bili ya umeme kwa mda alisema maeneja.

hivi ndiyo hali ilivyo

unaona nini ndani ya ndoo?
Mwisho

No comments:

Post a Comment