Saturday, September 5, 2015

KAMBI YA KITALII YAUNGUA MOTO, ROBANDA –SERENGETI.



KAMBI YA KITALII YAUNGUA  MOTO, ROBANDA –SERENGETI.

Na Samwel M.P

Leo siku ya J`mosi tarehe 05/09/2015 majira ya saa 5 asubuhi kuelekea saa 6 mchana, baadi ya majengo ya kambi ya kulala watalii ya Ikoma Safari Camp maarufu kama kwa Pepe iliyopo katika kijiji cha Robanada wilaya ya Serengeti  yameteketea kwa moto. Mwandishi wa Blog hii ameshuhudia kwa macho tukio hili ambapo alifika kambini hapo akiwa katika ziara yake ya kutembelea wadau wa Utalii hasa kambi za kulala wageni na kufanya mazungumuzo na uongozi na hata wafanyakazi wa kawaida wa kambi zinazopatikana eneo la Robanda na Ikona WMA.


Alipofika alikuta moshi mkubwa wa moto umetanda uliokuwa umesababishwa na kuungua kwa majengo hayo ya Kambi hiyo ya IKOMA Camp (kwa PEPE).  Akiongea na mwandishi wa blog hii, Meneja wa Kambi hiyo Bi. Tonel Brite amesema kuwa hata yeye anashindwa kubainisha kuwa ni nini chanzo cha moto huo kwa sasa mpaka pale uchunguzi utakapofanywa na timu ya wataalam wa majanga ya moto itakayokuwa imetumwa na kampuni inayomiliki Kambi japo tetesi za awali zinaonyesha kuwa ni hitilafu katika vyombo vyao vya umeme. Brite kwa maelezo yake mengine ya awali alisema kuwa yeye alikuwa ndani akiendelea na kazi ya kupitia vitabu vya mauzo na mlinzi aliekuwa zamu alikuwa ameenda kuzima mashine inayosukuma maji toka kisimani kuja kwenye kambi, ambapo mlinzi huyo wakati anaudi ndipo aliona moshi ulioashiria moto na alipoenda kuona alikuta tayari moto umeishaanza kuteketeza jengo na umeshika katika nyasi zilizotumika kuezekea majengo.

Mlinzi huyo ambae jina lake halikuweza kufahamika alimtaarifu meneja kuwa kuna moto na meneja pamoja na wafanyakazi wengine wa kambi hiyo walipiga (mwenu) yoe au kelele kwa kuwaita watu ambao wako maeneo jirani na kambi hiyo kwa ajili ya kuomba msaada wa kudhibiti moto; majirani wa kambi walijitokeza na kusaidia baadhi ya vitu vichache toka kwenye majengo yaliokuwa yameshika moto. Kwa mujibu Bi, Brite ambae ni meneja wa kambi, amesema kuwa vifaa vingi vimeteketea kwa moto, na kusema jingo lililoteketea ni ambalo linatumika kama Baa, Bwalo la chakula (Mesi) na Jiko. Haya ni maeneo   ambayo yanakuwa na vifaa vingi vya huduma, mapambo ya gharama, fenicha (Samani), n.k hivyo ndiyo maana nasema vitu vingi vimeungua alisema Brite.

Hakuna mtu yeyote alieripotiwa kujeruhiwa au kupoteza maisha kutokana na moto huo. Kuhusu hasara ambayo kambi hiyo imeipata kutokana na janga hilo la moto Bi. Brite amesema haizi kulisemea hilo kwa sasa mpaka pale tadhimini itakapofanywa badae na uongozi wa kampuni. Pia ikumbukwe kuwa miezi kama 2 iliopita, aliekuwa meneja msimamizi na mwanzilishi wa kambi hiyo Bw. PEPE alifariki dunia hivyo bado wafanyakazi wanamajonzo ya kuondokewa na mwanzilishi wa kambi hiyo.

Kutokana na ziara ya mwandishi wa Blog hii ya kutembelea kambi zinazopatikana Robanda, nyingi zimeonekana kuwa katika hatari kubwa ya kunguua moto kutokana na uchomaji wa moto unaofanywa na watu wasiojulikana kwenye maeneo yanayozunguka kambi hizo. Uongozi wa kambi hizo umedai mara nyingine moto hutokea ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mwingine kuchomwa na wanakijiji kwa lengo la kuchoma mkaa na kuweka mitego yao ya kunasa wanayama aina ya Swala ambao huvutiwa na nyasi change zinazochipua baada ya kuchoma moto. Tunakosa amani na tunakosa raha kwa hofu ya moto hasa nyakati za kiangazi kikali, moto unaibuka gafla ni changamoto kubwa sana alisema Bw. Timoth wa Mapito camp


 
Jengo la Restaurant ambalo lilikua na kigorofa likiwa limeteketea kwa moto

Wanakiji wakiwa wanaendelea kuokoa vyombo mbalimbali toka ndani huku wengine wakianza kulewa kwa kunywa mivinyo ilikutwa Baa, wengine wakila matunda na kulamba sukari ili waongeze nguvu ya kuukabili moto

Vyombo vinaendelea kutolewa nje, kama inavyoonekana.

Sasa siyo gorofa tena ila ni majivu

Kazi ni moja tu kuzima moto.

Niwahishie maji, alisema huyo mzima moto.


Charle nae alikuwepoo

Moto lazima uzimike.

.

No comments:

Post a Comment