Saturday, September 3, 2016

TATIZO LA MAJI MUGUMU/SERENGETI BADO NI KITENDAWILI.



TATIZO LA MAJI MUGUMU/SERENGETI BADO NI KITENDAWILI.

Na Samwel M.P

03/09/2016

Ndivyo tunavyoweza kusema kuwa tatizo hili la maji katika mji wa Mugumu na viunga vyake kuwa sasa ni kitendawili amabacho kinahitaji kuteguliwa na mamlaka zote husika kwa haraka  ili kuwanusuru wananchi na hatari ya milipuko ya magonjwa amabayo yanaweza kujitokeza kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani. Lakini pia inavyoelekea kitendawili hiki kinaweza kisiteguliwe kwa wakati kama hakutakuwepo na msukumo/shinikizo la kutoka kwa wananchi wenyewe ambao ndio wahanga wa tatitizo hili kwa kusaidiwa na mwakilishi wao bungeni ambae ni mbunge wa jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba, Serengeti ONLINE imebaini.

Kwa mujibu wa taarifa ya mhandisi wa maji wilaya, Eng. Marwa Mlaza, tatizo hili la kukosekana kwa huduma ya maji kwa wananchi wa Mugumu, lilianza tangu tarehe 09/05/2016 ambapo pump ya kusukuma maji toka bwawa la manchira iliungua. Mchakato wa kupata mkandarasi na kuwagiza pump mpya na motor chini ya mamlaka ya maji Musoma –MUWASA ulifanika na hadi sasa zoezi hilo halijakamilika kutokana na motor kungua mara mbili. Hivyo basi ifikapo tarehe 09/09/2016 itakuwa imekamilika miezi 4 mfululizo sawa na siku 120 bila maji kwa wananchi na wakazi wa mji wa Mugumu, jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na mazingira yake vilevile.

Leo sept. 03, mwandishi wa blog hii ametembelea Manchira ambako kulitarajiwa kuwa na zoezi la kufunga motor kwa ushirikiano wa watalaam toka wizara ya maji (Dsm), MUWASA (Musoma), Supplier wa Motor (Arusha) na mafundi wa MUGUWASA na H/Mashauri ya wilaya Serengeti; zoezi hili limeshindwa kufanyika na watu kutawanyika kutokana na sababu zifuatazo kama ilivyoelezwa:-

1)   Hapakuwepo na mwakilishi au mtalam toka upande wa supplier wa motor kutoka arusha, na alipotakiwa kutoa ithini ili mafundi wa wizara na MUWASA kuendelea na ufungaji wa motor alikubali kwa maneno kupitia simu, na badae wakamuomba akubali kwa  maandishi kupitia barua pepe (email) kama sehemu ya kuweka kumbukumbu, mkandarasi alikataa na kusema wamsubiri hadi siku ya jumatano  Sept. 07 ndiyo anaweza kutuma mafundi wake kuja Mugumu jambo ambalo pia linaweza kuwa sii la ukweli kama ilivyodaiwa kuwa amekuwa akiahidi uongo mara nyingi.

2)   Ilionekana kifaa cha mambo ya umeme (circuit breaker) chenye capacity ya 180 A brand ya ABB ambacho kinatakiwa kufungwa kwenye mfumo wa umeme wa motor hiyo pia hakipo, na kilitakiwa kuwagizwa aidha Musoma au kuingine; hii ni baada ya mkandarasi kuwambia kuwa amekituma kwa ndege toka arusha kuja seronera na baada ya kufika seronera kwa bahati mbaya tena ndege imerudi nacho arusha baada ya kukosewa jina la mpokeaji.
3)   Tatu, ilikuwa tu ni vifaa vingine vidogo vidogo vilivyoshauriwa na mtaalam toka wizani kuwa ni vyema vikafungwa hapo ili kukomesha tatizo hilo kujirudia hasa katika mfumo wa umeme, vitu ambavyo pia inaonekana vinahitaji fungu Fulani ili kuletwa.

Katika mahojiano ya hapa na pale, ilionekana kuwa Mkurugenzi wa MUWASA ndiye anapaswa kumbana mkandarasi kwani MUWASA ndiyo iliyosaini mkataba na mkandarasi. Akiongea kwa masikitiko mwakilishi wa wizara ya maji (jina halikupatikana) amesema, MUWASA ni mamlaka kamili, hivyo wao kama wizara wanakosa nguvu ya kuingilia jambo hilo na kumforce mkandarasi, ila watajaribu kumshauri MUWASA kuona namna ya kumbana supplier ili afike mapema badala ya hiyo anayosema jumatano; na timu yake ya wizara haitondoka mpaka tatizo limekuwa solved; huku akihofia kuwa endapo itafika sept. 06 kabla ya maji kutoka, kuna hatari ya waziri wa maji kupata wakati mgumu bungeni toka kwa Mbunge wa Serengeti.

Pamoja na mambo mengine, watalamu wa wizara na Muwasa pia kila mmoja wameonyesha kushangaa jinsi wanamugumu walivyo kimya  huku wakiwa na tatizo kubwa kama hili. Mmoja wao amesema yeye alikusudia angefika akakuta (Nyomi ya watu) yaani kundi kubwa la wananchi wakiwa bwawani kama sehemu ya kudai kupata huduma ya maji, kama alivyowahi kushuhudia katika miji mingine aliowahi kufika kwa kesi kama hii. “Miezi 4 bila maji sii jambo dogo”, alisema. Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, motor haikufungwa na kila mmoja alionekana kumtupia lawama supplier na mafundi wote wa muwasa na wizara wameondoka kuridi musoma hadi siku watakapofika mafundi wa supplier.

==Mwisho==
Kazi inaendelea.

Gari ya MUWASA iliokuja na mafundi wa MUWASA na wale wa kutoka wizara ya maji (dsm)

Baada ya zoezi kuahirishwa, kazi ikawa ni kurudisha motor stoo


Makatibu wote wawili wa Mbunge, wa kiwasaidia mafundi kurudisha motor stoo, inaonekana ndogo ila ina uzito karibu 300kg



No comments:

Post a Comment