SIKU YA MAZINGIRA AFRICA.
Kutokana na
kuongezeka kwa Idadi ya watu katika nchi mbalimbali Duniani shughuli za
kiuchumi nazo zinakuwa na kuongezeka kulingana na hali halisi ya watu
(population), wakati Idadi ya watu ikiongezeka na shughuli za kiuchumi kwa kila
nchi huongezeka na hali ya mazingira inazidi kuwa tete kwa kuchafuliwa kutoka
na shughuli za uzalishaji za kila siku zinazofanywa eitha na mtu mmoja mmoja au
Viwanda.
Kutokana na
hali hiyo, Nchi wanachama wa Africa (AU) ziliona ni muhimu kuwa na utaratibu na
mpango wa kuokoa mazingira katika nchi mwanachama wa AU. Nchi hizi kwa pamoja
ziliridhia uanzishwaji wa wiki ya mazingira Barani Africa ambayo kilele chake
huadimishwa kila tarehe 03 machi kila mwaka ambapo siku hii watu wote hutakiwa
kushiriki katika shughuli za kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya
makazi, maeneo ya Biashara kama masoko, Viwanda n,k hii ni kwa ajili ya
kuyaweka mazingira safi kwa ajili ya ustawi wa Binadamu ambao afya zao zaweza
kuwa hatarini kama matekeo ya mazingira kuwa machafu.
Siku hii ya
mazingira barani afrika huadhimishwa na kila nchi mwanachama wa AU kupitia
serikali zake, kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali, Asasi/Mashirika ya
kiraia pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira ambapo hii inaweza kufanywa kwa
staili tofautofauti kulinga na utashi wa Serikali na wadau wengine kwa kila
nchi bila ya kubadili maana halisi ya siku hii ya machi,03.
HALIMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI
YADIMISHA SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA
Halimashauri
ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara kupitia Idara yake ya Mazingira imeadimisha
siku ya usafi wa mazingira barani Afrika kwa watumishi wa halimashauri hii
kutoka ofisini na kuungana na wananchi wengine kufanya usafi katika maeneo ya
mji wa Mugumu ambao ni makao makuu ya halimashauri hiyo ya Serengeti.
Katika kuhakiki
kuwa jamii inawelewa nini maana ya siku hii ya machi 03 H/M ilichukua jukumu la
kuweka matangazo ya wazi yaliotangazwa kwa njia ya Vipasa sauti kuzungu mji
mzima wa Mugumu na Vitongoji vyake kwa lengo la kuhasisha wananchi kushiriki
katika shughuli za usafi wakianzia na maeneo yao ya makazi (Nyumbani mwao) na
pia kushiriki katika zoezi la pamoja la kufanya usafi kuzunguka mji wa Mugumu,
zoezi ambalo liliongozwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti na mkurugenzi wa
Halimashauri ya wilaya.
Katika utekelezaji
wa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira watumishi wa halimashauri
wamejitokeza japo kwa uchache kuungana na wananchi wengine, WANAFUNZI WA CHUO
CHA UTALII CHA SERENGETI (SETCO) pamoja na WATUMISHI wengine wa chuo hicho
wamejitokeza na kuungana na wafanyakazi wa halimashauri ya wilaya na wale wa
kutoka katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Mugumu, wananchi wa kawaida wamejitokeza
kwa uchache sana ambao idadi yao haikuzidi watu 15 ukilinganisha idadi ya watu
walio katika mji wa Mugumu ambao ni zaidi ya watu 5000. Maeneo yaliopata bahati
ya kufanyiwa usafi ni pamoja na eneo la soko kuu ambalo limefanyiwa usafi na
wanafunzi na watumishi toka chuo cha SETCO na eneo la Uwanja wa mbuzi ambalo
limefanyiwa usafi na watu wote akiwepo mkandarasi wa usafi wa mji wa mugumu
ambae hata hivyo jina lake halikufahamika kwa haraka.
Nyenzo zilizotumika
katika zoezi hili muhimu la usafi zilikuwa ni pamoja na; Panga, Majembe,
sepeto, Rekki, mafekeo, mifagio, mikokoteni na Gari kwa ajili ya kubebea uchafu
kwenda jararani. Watu walifanya kazi ya kufyeka, kuokota na kupeleka uchafu
jararani.
MKUU WA WILAYA AONGEA NA WANANCHI:
Mara baada ya
zoezi la usafi kumalizika kwa mujibu wa ratiba iliokuwepo Kaimu Mkuu wa wilaya
ambae pia ni Afisa tawala wa wilaya ya Serengeti alipata fursa ya kuongea na
wanachi kama sehemu ya kutoa maagizo ya Serikali kuhusiana na siku hii ya
mazingira Afrika. Akiongea na wananchi kaimu mkuu wa wilaya Bw. Zonzo alisema
kila mwananchi kwa nafsi yake ana jukumu la kulinda na kuweka mazingira safi
kwa ajili ya ustawi wa jamii, alisema kwa kuwa shughuli za kiuchumi
zinaongezeka mazingira yanakuwa katika hatari ya kuharika kutokana na shughuli
hizo hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuona umuhimu wa kulinda mazingira kwa
kufanya usafi kama inavyotakiwa.
Bw. Zonzo
hakuishia hapo ila alisema pia wadau wa mazingira wafanye jitihada za
kuendeleza maeneo ya wazi katika mji wa Mugumu akitolea mfano eneo la uwanja wa
Bunzi kuwa linafaa sana kuwekewa Bustani (Garden) ya kupumzikia watu huku
wakipata kinyaji bila kutaja ni kinywaji cha aina gani. Mkuu wa wilaya pia
amekerwa na tabia ya wananchi walio wengi kupuuzia swala hili la usafi wa
mazingira ambapo watu hawakutokea na badala yake walibaki kuwashangaa wale
waliokuwa wakifanya zoezi la usafi, Mkuu huo aliongeza kwa kibwagizo kidogo
kuwa “nashangaa kuona watu wanambia kuhusu habari ya kufanya usafi hawajitokezi
badala yeke wamebaki kuwashangaa nyie mliojitokeza lakini wangeambia mtu
kashikwa ugoni hapa uwanja ungepungua “ alisema
Mwisho mkuu wa
wilaya alimaliza kwa kutoa ushauri ambao kimsingi ulichukuliwa kama agiizo
rasimi la serikali kuwa wilaya kupitia wataalamu wake wa mazingira wafanye
utaratibu wa kufanya usafi wa mazingira kwa kila wiki, pia aliagiza watu ambao
ni vinara wa kuchafua mazingira wakamatwe bila ya kuwaogopa na wafikishe
mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake, “watuwezi kuvumilia watu wanachafua
mazingira wazi wazi huku hawachukuliwi hatua zozote kwa sababu wao ni maarufu
hapa mjini” alisema Bw. Zonzo
| wanafunzi wa chuo cha SETCO wakiokota Uchafu eneo la soko kuu mjini mugumu |
| usafi eneo la uwanja wa mbuzi |
| Soko kuu wanafunzi wa STCO wakizoa uchafu |
| wa kwanza kushoto ni kaimu DC serengeti Mr. Zonzo, katikati baada ya mwanamke ni kaimu DED serengeti wa kwanza kulia ni Afisa Mazingira wilaya Victor Charles |
| Afisa wanyama pori W Mr. Cathbet Boma akifyeka eneo la uwanja wa mbuzi |
No comments:
Post a Comment