Kwa
zaidi ya kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita, wananchi wa wilaya ya
Serengeti na mkoa wa Mara kwa ujumla wamekuwa wakiishi kwa matumaini ya kupata
uwanja wa ndege wa kimataifa (International Airport) au wenye hadhi ya kati
(Standard airport); ambao kwa mujibu wa kauli za wanasiasa na viongozi wa
halmashauri ya (w) Serengeti, ulikuwa
ujengwe katika kijiji cha Burunga, kata ya uwanja wa ndege ambayo imo ndani ya
mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu kilometa chache toka hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Uwanja huu wa Serengeti ulikusudiwa kuwa moja ya vichocheo vya ukuaji wa maendeleo
hasa katika sekta ya usafirishaji na Utalii ndani ya wilaya ya Serengeti, mkoa
wa Mara na hata kanda ya ziwa kama mradi huu ungeweza kutekelezwa pamoja na
barabara ya makutano- Natta –Mugumu –Klensi – Loliondo Arusha kama wananchi
walivyokuwa wakiahidiwa katika majukwaa.
Kilichojiri
leo (15/02/2016) katika kikao cha baraza la madiwani wa H/m ya (w) Serengeti
ambacho kimeketi kwa ajili ya kupitia na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya H/M
kwa mwaka wa fedha 2016/2017, jambo hili la uwanja wa ndege wa Serengeti
limeibuka kwa sura ambayo haikutegemewa na kuleta hisia tofauti na maswali
mengi kwa wananchi na hata madiwani wenyewe. Hii ni baada ya diwani wa kata ya
uwanja wa ndege Mhe. Daniel Kegocha (CCM) maarufu kama (Maisa) kutaka kupata
ufafanuzi wa kina toka kwa katibu tawala wa mkoa Mara ambae alikuwepo kwenye
kikao hicho, kuhusiana na kukwama kwa utekelezaji wa mradi kwa mda mrefu na
kusadikiwa kuwa mradi huo unakwamishwa na uongozi wa mkoa hasa ofisi ya Mkuu wa
mkoa wa Mara, pamoja na kwamba taratibu zote zilishakamilika.
Akitoa
ufafanuzi wa jambo hilo, RAS – Mara amesema kuwa, jambo hilo la uwanja wa ndege
halipo mkoani na wala ofisi ya RC haina nia yoyote mbaya ya kukwamisha mradi
huo kama inavyodaiwa isipokuwa bado jambo hilo liko halimashauri ya Serengeti.
RAS akasema mkoa unashughulika na uwanja wa Musoma ambao ni miongoni mwa
viwanja 12 vya ndege vya Tanzania ambavyo vilingia katika mpango wa kujengwa
kupitia mkopo wa World Bank ukiwemo uwanja wa ndege wa Bukoba ambao amesema
umeishajengwa. Akaongeza kusema kuwa serekali kuu haiwezi kujiingiza katika
swala ambalo bado halijatimiza vigezo kwa maana ya kufuata taratibu zote husika
kama inavyotakiwa kisheria.
WITO wa RAS kwa
halmashauri ya Serengeti:
ameushauri uongozi wa H/M kupitia baraza hilo kuwa, kama h/m inapenda
kufanikisha jambo hilo wawe na vitu vifuatavyo;
- Mkataba halali baina ya H/M na mwekezaji alieonyesha nia ya kusaidia ujenzi wa uwanja na uonyeshe wazi ushiriki (commitment) ya mwekezaji na uonyeshe wazi mwekezaji anagarimia asilimia ngapi za gharama za mradi
- H/M ionyeshe chanzo kingine cha fedha za kugarimia mradi na nikiasi gani ambacho wanakusudia kukipata toka kwa chanzo hicho ambacho kinaweza kuwa ni pamoja na wadau wengine wa maendeleo toka ndani na nje ya wilaya.
- H/M ipeleke ombi hilo TAMISEMI, lipite tume ya Mipango, lipite kwa idara inayohusika na utekelezaji wa miradi ya ubia (PPP), mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) n.k
Ameongeza
kwa kusema kuwa endapo hayo kifanyika basi itakuwa ni rahisi kwa jambo hilo
kuweza kusonga mbele kwani litakuwa limeeleweka muundo wake na kupata Baraka zote.
Nawashauri jambo hilo lifanyike by 2018/2019 kwa sababu kwa sasa 2016/17 mda
umeisha. “amesema RAS”
Baada
ya melezo hayo ya RAS, hakuna diwani aliyeweza kutoa mchango wowote kuhusiana
na swala hilo pengine kwa jinsi anavyolifahamu kutokaa na ushahidi wa mambo
mbalimbali yaliowezakuwa yakifanyika hapo awali kwa ajili ya swala la uwanja
hasa madiwani waliokuwepo katika kipindi cha awamu iliopita na sasa
wamefanikiwa kurudi kwenye baraza; wote walikua kimya. Lakini pia baada ya
maelezo hayo ya RAS imeonekana dhahiri kuwa jambo hilo la uwanja wa ndege
Serengeti bado ni wazo (Idea) ambalo lilikuwemo na limo ndani ya vichwa vya
watu Fulani au viongozi wa juu wa h/m, lakini wao wakalileta kwa wananchi kwa
sura kama ni kitu ambacho kikotayari na kinaenda kuwa implemented soon, kama
kweli hakuna zengwe lolote nyuma ya pazia.
MASWALI
YA WANANCHI:
- Kama ndivyo ilivyo, je ni kwa nini viongozi walionekana kufanya ziara za kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji wa viwanja kana kwamba swala hilo liko tayari?
- Je walikua wakitumia fedha za umma au zao binafsi katika kufanya ziara hizo?
- Je uko wapi mkataba pamoja na file lote la mradi uliosemwa kuwa tayari h/m ina mkataba na mwekezaji katika kujenga uwanja wa Serengeti?
- Je ni kwanini h/m iliamua kufidia wananchi wa Burunga kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege Serengeti?
- Kama hapo awali ilionekana kuwa taratibu zimekamilika kiasi cha kutangazia wananchi je, inakuaje leo inaonekana hakuna kilichofanyika?
Mpaka
mwandishi wetu anaondoka eneo la h/m hayo ndiyo maswali ambayo wananchi na
madiwani wapya walikuwa wakijihoji na kutaka ipatikane namna ya kupata majibu
ya maswali hayo toka kwa viongozi wanaofahamu swala hilo.

Da kumbe kuna madudu namna hii
ReplyDelete0K
ReplyDelete